Friday, July 13, 2012

KEWELL ATEULIWA KUWA MWANAMICHEZO BORA WA KIPINDI CHOTE NCHINI AUSTRALIA.

Harry Kewell.
NYOTA wa zamani wa klabu ya Liverpool na Leeds United, Harry Kewell amepigiwa kura nchini kwao Australia kuwa mchezaji bora ambao hajapata kutokea kwa nchi hiyo. Kewell alitunukiwa tuzo hiyo ambayo iliamuliwa kwa kura za wananchi na maoni ya jopo la wataalamu katika sherehe zilizofanyika Alhamisi jijini Sydney. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye kwasasa amerejea Uingereza baada ya kucheza msimu mmoja katika klabu ya Melbourne inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo maarufu A-League, hakuwepo kupokea tuzo hiyo. Kewell amesema kuwa kitendo cha kutajwa kama mmoja wachezaji bora kuwahi kutokea nchini humo ni kitu ambacho kamwe hawezi kukisahau katika maisha yake na aliwashukuru wote waliofanikisha shughuli hiyo pamoja na mashabiki waliompigia kura. Kura zaidi ya 15,000 zilihesabiwa katika uchaguzi huo wakati jopo la wachezaji wa sasa na wazamani, watendaji na wachambuzi mbalimbali pia walisaidia zoezi hilo la kumchagua mshindi.

No comments:

Post a Comment