LAVAGNE ATAKA ETO'O AVULIWA UNAHODHA CAMEROON.
 |
Samuel Eto'o. |
KOCHA wa timu ya taifa ya Cameroon, Denis Lavagne anataka mshambuliaji wa timu hiyo ambaye pia ni nahodha Samuel Eto’o avuliwe unahodha wakati ataporejea katika timu hiyo baada ya kumaliza kifungo chake baadae mwaka huu. Eto’o alifungiwa miezi nane kwa kuongoza mgomo Novemba mwaka jana wakati Cameroon ilipokataa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Algeria wakidai posho zao za ziada ambazo walikuwa hawajalipwa. Katika barua iliyotumwa kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo, Lavagne ambaye ni raia wa Ufaransa alilitaka shirikisho hilo kutoa maamuzi juu ya kuchagua nahodh mwingine kabla ya mchezo dhidi ya visiwa vya Cape Verde utakaofanyika Septemba na Oktoba mwaka huu wa kufuzu mzunguko wa mwisho wa michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani. Katika barua hiyo Lavagne pia alilalamikia shirikisho hilo kwa kutomlipa mshahara wake wa mwaka ambao unafikia kiasi cha dola 245,000 kwani mkataba wake unaainisha kuwa ni lazima apewe kiasi hicho kwa ujumla. Lavagne ambaye katika siku za karibuni alionywa na shirikisho hilo baada ya kuonysha utovu wa nidhamu mbele ya waziri wan chi hiyo alichaguliwa kuinoa timu hiyo mwaka uliopita kuchukua nafasi ya Javier Clemente wa Hispania ambaye alitimuliwa baada ya kushindwa kuipeleka timu hiyo kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment