SAUDI ARABIA KUPELEKA WANARIADHA WAWILI WA KIKE OLIMPIKI.
 |
Sarah Attar. |
KAMATI ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC imesema kuwa nchi ya Saudi Arabia inatarajiwa kupeleka wanariadha wawili wanawake kwenda kushindana katika michuano ya olimpiki inayotarajiwa kufanyika jijini London, Uingereza mwaka huu. Wanariadha hao ni Sarah Attar ambaye atashindana katika mbio za mita 800 na Wodjan Ali Seraj Abdulrahim Shahrkhani ambaye atashiriki katika mchezo wa judo katika michuano hiyo. Mamlaka ya nchi hiyo iliondoa sheria ya kuwazuia wanawake katika ukanda huo wa Gulf kushiriki michezo yoyote mwezi uliopita. Lakini ushiriki wa wanawake katika michezo ya jumuiya bado inapingwa vikali na waumini wenye misimamo mikali nchini Saudi Arabia. Rais wa IOC, Jacques Rogge amesema kuwa hiyo ni hatua nzuri kwasasa na anaamini huko mbele wataweza kutuma wanariadha wengi zaidi wanawake katika michuano hiyo ya kihistoria. Akiongea wakati akiwa katika kambi yake ya mazoezi nchini Marekani, Sarh Attar amesema kuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi yake na anaamini wanawake wengi watahamasika kujiunga katika michezo.
No comments:
Post a Comment