Friday, July 13, 2012

WATU NANE WAFA WAKATI PALMEIRAS WAKISHANGILIA USHINDI.

Louis Felipe Scolari, Palmeiras coach.
 WATU wanane wamepigwa risasi na kufa katika wilaya tofauti kwenye jiji la Sao Paulo mapema Alhamisi wakati mashabiki wa soka wa klabu ya Palmeiras wakishangilia ushindi wao wa Kombe la Ligi nchini Brazil. Polisi wamesema kuwa watu tisa ndio walipigwa risasi ambapo nane kati yao walifariki dunia katika mji mdogo wa Osasco ambao ni wa tano kwa kuwa na watu wengi kwenye jiji hilo kubwa la Sao Paulo. Katika taarifa iliyotolewa na polisi imesema kuwa watu waliofanya tukio hilo walisubiri wakati mashabiki wa Palmeiras wakifyatua mafataki kusherehekea ushinda na wao kutumia mwnya huo kufanya tukio hilo. Lakini taarifa hiyo ilisisitiza kuwa mauaji hayo hayahusiani na ushindi iliyopata timu hiyo kama watu wengi walivyokuwa wanafikiri kwani katika watu waliokufa hakuna yoyote ambaye alikuwa amevaa jezi ya timu ya Palmeiras. Katika wilaya hiyo ya Osasco inayokaliwa na watu wanaokadiriwa kufikia 680,000 ambayo inafahamika kwa biashara haramu za madawa ya kulevya takwimu zinaonyesha watu 11 hufa kwa kuuliwa kila mwezi katika matukio tofauti.

No comments:

Post a Comment