Wednesday, July 11, 2012

NOTTINGHAM FOREST YANUNULIWA NA WANAFAMILIA WA KUWAITI.


FAMILIA ya Al-Hasawi ya Kuwaiti imekamilisha mpango wa kuinunua klabu ya Nottingham Forest ambao wameshawahi kuwa mabingwa wa kombe la Ulaya mara mbili. Katika taarifa iliyotolewa na mtandao wa klabu hiyo Jumanne wanafamilia hao ambao ni Fawaz, Abdulaziz na Omar al-Hasawi wamesema kuwa watakutana na wandishi wa habari Jumamosi katika uwanja wa timu hiyo ili kutangaza taarifa hizo rasmi. Mfanyabiashara Fawaz Al-Hasawi alijiuzulu wadhfa wake kama mwenyekiti wa klabu ya Al-Quadisya mapema mwaka huu ili kujisafishia njia ya kuinunua Forest kutoka kwa aliyekuwa mmiliki w klabu hiyo ambaye ni marehemu Nigel Doughty. Wanafamilia wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa mbele yao ili kurudisha heshima ya klabu hiyo iliyokuwa nayo kipindi cha nyuma na kuomba ushirikiano kwa wadau na wapenzi wa timu hiyo kuwaunga mkono. Forrest waliwahi kuwa mabingwa wa soka wa Ulaya mwaka 1979 na 1980 lakini kwasasa klabu hiyo inacheza katika ligi daraja la pili nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment