
Thursday, July 12, 2012
PETERSEN ALIA NA MASHABIKI WA aFRIKA KUSINI KUACHA KUANGALIA MECHI ZA SOKA KWENYE LUNINGA.
OFISA Mkuu wa Chama cha Soka cha Afrika Kusini-SAFA, Robin Petersen amesema kuwa mashabiki wa soka wa nchini inabidi kuachana na suala ya kuangalia mipira ya moja kwa moja katika luninga ili viwanja vilivyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2010 visikose mashabiki. Petersen amesema kuwa mechi nyingi za soka huwa zinaonyeshwa moja kwa moja katika luninga hivyo hata watu wamebadilisha aina ya maisha badala ya kwenda uwanjani wengi wanakaa nyumbani kutazama mechi. Aliendela kusema kuwa watu wanatakiwa wabadilike na kuacha kukaa majumbani kutazama mechi na badala yake kwenda viwanjani hususani katika michuano ya Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza kufanyika mwakani nchini humo. Uwanja uliopo jijini Cape Town ambao haitatumika katika michuano ya Afrika mwakani unatajwa kama moja viwanja ambavyo havitumiki ipasavyo hivi sasa. Ofisa huyo ameendelea kusema kuwa viawanja pekee ambavyo vinaendelea vizuri kwa matukio mengi ya kimichezo na burudani kufanyika ni Uwanja wa Soccer City uliopo jijini Juhannesburg na Uwanja Peter Mokaba uliopo jijini Polokwane.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment