Thursday, July 12, 2012

TUSKER WAANIKA SILAHA WATAKAZOTUMIA KAGAME.

Joseph Emeka.
MCHEZAJI wa kimataifa wa Nigeria, Joseph Emeka, Keneth Wendo na Charles Odette ni miongoni mwa majina ya wachezaji wa timu ya Tusker ya Kenya ambao wameachwa katika kikosi cha kocha Sammy Omollo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame. Meneja wa timu hiyo amesema kuwa Emeka ametemwa kutokana na kushuka kwa kiwango chake wakati Wendo ameachwa kutokana na kuwa majeruhi hivyo hawezi kuwa tayari kwa ajili ya michuano hiyo. Katika kikosi hicho pia atakosa aliyekuwa beki wake Brian Mandela ambaye amehamia katika timu ya Sanlam Santos huku kukiwa sura mpya kwenye kikosi hicho cha wachezaji 20 kama Allan Kateregga, David Makumbi Nyanzi na Joshua Oyoo. Tusker ambayo imepangwa kundi moja na timu za Azam na Mafunzo inatarajiwa kutua nchini Jumapili tayari kwa michuano hiyo kikiwa na makipa Boniface Oluoch and Samuel Odhiambo, mabeki Jockins Atudo, Humphrey Okoti, Joseph Shikokoti na Luke Ochieng. Wengine ni Jerry Santo, Peter Opiyo, Fredrick Onyango, Obadiah Ndege, Maurice Odipo, David Ochieng, George Opiyo, David Makumbi Nyanzi, Joseph Mbugi, Dennis Mukaisi, Andrew Murunga, Patrick Kagogo, Allan Kateregga, Joshua Oyoo.

No comments:

Post a Comment