![]() |
Tom Saintfiet. |
Kocha huyo amesema kuwa pamoja na kumtema Nsajigwa katika kikosi hicho lakini mchezaji huyo bado ni muhimu katika timu hiyo na ameamua kumpa nafasi ya kujiweka fiti kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambako atamtumia. Kikosi kamili cha Yanga ambacho kitashiriki Kagame kitakuwa na makipa Yaw Berko na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki watakuwa Juma Abdul, David Luhende, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Oscar Joshua na Stefano Mwasika. Wengine ni viungo Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid Gumbo, Juma Seif ‘Kijiko’, Haruna Niyonzima, Shamte Ally, Nizar Khalfan na Idrisa Assenga wakati washambuliaji watakuwa ni Said Bahamuzi, Hamis Kiiza na Jerry Tegete. Saintfiet amesema kuwa kiungo Nurdin Bakari naye ametemwa katika kikosi hicho kutokana majeraha yanayomsumbua ambapo daktari wa timu amesema ataweza kuwa fiti baada ya wiki mbili wakati ambao michuano ya Kagame itakuwa tayari imeshaanza ndiyo sababu kubwa ya kuachwa.
No comments:
Post a Comment