KHAN KUTETEA MKANDA WAKE WBA JUMAMOSI.
 |
Amir Khan. |
MWANAMASUMBWI nyota kutoka Uingereza Amir Khan ambaye amerejeshewa mkanda wake wa WBA uzito wa light-welterweight anatarajiwa kuuweka mkanda huo rehani pale atakapochuana na bingwa wa WBC wa uzito huo Danny Garcia jijini Las Vegas, Marekani Julai 14 mwaka huu. Khan alipoteza mikanda yake ya WBA na IBF baada ya kupigwa na Lamont Peterson Desemba mwaka jana katika pambano lililokuwa na utata. Bondia huyo amesema kuwa hatimaye haki imepatikana kwa WBA kumrejeshea mkanda wake na pambano lake dhidi ya Garcia litaonyesha nani ni bingwa katika uzito huo wanaopigania. Khan alikata rufani kufuatia kuzidiwa kwa alama moja kwenye mchezo huo dhidi ya Peterson ambapo WBA walimrudishia mkanda huo kutokana na baadhi kasoro zilizoonekana katika pambano hilo.
No comments:
Post a Comment