Wednesday, July 18, 2012

VILLAS-BOAS AMNYATIA HULK.

MENEJA wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Andre Villas-Boas ameingia katika kinyang’anyiro cha kumgombea mshambuliaji wa klabu ya porto ya Ureno Hulk. Hulk yumo katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki ambacho kimewasili jana jijini London tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya Uingereza utakachezwa mwishoni mwa wiki hii. Villas-Boas ambaye amewahi kumfundisha mchezaji huyo wakati akiwa kocha wa Porto ameonyesha nia ya kumleta Spurs yenye maskani yake katika Uwanja wa White Hart lane na tayari klabu hiyo imemruhusu kuanza mazungumzo na mchezaji huyo. Mbali ya Hulk Spurs pia wameonyesha nia kwa mchezaji wa Intercional ya Brazil, Leandro Damiao pamoja na kiungo wa Fluminense Wellington Nem na Manuel Lanzini ambaye baye tuko katika klabu hiyo hiyo. Hatahivyo usajili mpya uliokamilika wa Jan Vertonghem unaweza kuwasaidia klabu hiyo kufukuzia taji la Ligi Kuu nchini Uingereza mwaka huu baada ya kulikosa msimu uliopita kwa kumaliza narfasi ya nne.

No comments:

Post a Comment