ABIDAL ATEGEMEA KUREJEA UWANJANI DESEMBA.
|
Eric Abidal. |
BEKI wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Ufaransa, Eric Abidal ambaye kwasasa anapona kutokana na upasuaji wa kupandikizwa ini jingine Aprili mwaka huu amesema kuwa anatarajia kurejea uwanjani Desemba mwaka huu. Akizungumza mara baada ya mchezo baina ya Barcelona na Paris Saint-Germain uliofanyika jijini Paris ambapo klabu yake ilishinda mabao 4-1 katika changamoto ya mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida, Abidal amesema kuwa ameshaanza mazoezi ya gym na anajisikia vyema. Anasema ana safari ndefu ya kupona kabisa hivyo anatarajia kurejea uwanjani Desemba lakini kama atahitaji kuendelea kusuburi zaidi ya muda huo ili awe kurejea uwanjani haitakuwa tatizo kwake kwani atafanya hivyo. Beki huyo aliendelea kusema kuwa kwasasa anajisikia vyema kuliko miezi mitatu iliyopita na amekuwa akifuata masharti aliyopewa na madaktari waliomtibu. Abidal mwenye umri wa miaka 32 alifanyiwa upasuaji April 10 mwaka huu ikiwa ni mwaka mmoja kupita toka alipoondolewa uvimbe katika ini lake Machi mwaka jana ambapo aliruhusiwa Mei kutoka hospitalini jijini Barcelona.
No comments:
Post a Comment