Sunday, August 5, 2012

SERENA, VENUS WANYAKUWA DHAHABU OLIMPIKI.

Serena na Venus Williams wakipongezana mara baada ya kushinda medali ya dhahabu.
WACHEZAJI nyota wa mchezo wa tenisi Venus na dada yake Serena Williams wamefanikiwa kunyakuwa medali ya dhahabu katika mchezo huo wawili wawili na kuwa ndugu wa kwanza kushinda michuano hiyo mara tatu. Pamoja na kucheza chini ya kiwango chao ndugu hao raia wa Marekani walifanikiwa kuwafunga Andrea Hlavackova na Lucie Hradecka kutoka Jamhuri ya Czech kwa 6-4 6-4. Mara ya kwanza wawili hao walishinda michuano ya wawili wawili ya olimpiki iliyofanyika Sydney mwaka 2000, hawakuweza kutetea taji lao katika michuano ya mwaka 2004 kutokana na Serena kuwa majeruhi lakini walifanikiwa kunyakuwa taji hilo tena katika michuano ya Beijing mwaka 2008.
Tiki Gelana.



Kwa upande mwingine mwanadada mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Ethiopia Tiki Gelana amefanikiwa kushinda mbio hizo za kilometa 42 kwa kuweka rekodi ya olimpiki ya muda wa saa 2 dakika 23 na sekunde saba. Nafasi ya pili imekwenda kwa mwanadada kutoka Kenya Priscah Jeptoo wakipishana sekunde tano na Gelana huku nafasi ya tatu ikienda Urusi kwa Tatyana Petrova.

No comments:

Post a Comment