FELIX ANYAKUWA MEDALI YA DHAHABU MBI ZA MITA 200.
|
Allyson Felix. |
MWANARIADHA nyota wa Marekani mwanadada Allyson Felix amefanikiwa kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki yam bio za mita 200 akitumia muda wa sekunde 21.88 na kuwa taji lake la tatu katika michuano mitatu tofauti. Felix ambaye ni bingwa mara tatu wa wa dunia alifanikiwa kunyakuwa medali yake ya kwanza ya dhahabu katika michuano ya olimpiki baada ya kushindwa kufanya hivyo katika michuano ya olimpiki ya mwaka 2004 na 2008 ambayo yote aliambulia medali ya fedha. Mwanadada huyo ambaye ni raia wa Marekani alichuana vikali na Shelly-Ann Fraser-Pryce wa Jamaica ambaye alipata medali ya fedha akitumia muda wa sekunde 22.09 wakati nafasi ya tatu ilishikiliwa na Mmarekani mwingine Carmelita Jeter aliyetumia muda wa sekunde 22.14. Mbio za mita 200 zitaendelea tena leo ambapo bingwa mtetezi Usain Bolt anatarajiwa kutetea medali yake hiyo baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali jana akiongoza kwa kutumia muda wa sekunde 20.18. Mpinzani mkubwa wa Bolt katika mbio hizo ambaye wote wanatoka Jamaica na kufundishwa na mwalimu mmoja Yohane Blake naye ametinga katika hiyo akitumia muda sekunde 20.01 na kuonyesha kuwa fainali hiyo itakuwa na ushindani mkubwa.
No comments:
Post a Comment