FIFA YAMCHUNGUZA TENA BIN HAMMAM.
|
Mohamed bin Hammam. |
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeanza uchunguzi mpya wa mgombea wa zamani wa urais wa shirikisho hilo Mohamed bin Hammam ikiwa haujapita hata mwezi toka Mahakama ya Usuluhisho ya Michezo-CAS kutengua adhabu ya kufungiwa maisha kujishughulisha na michezo. Uchunguzi huo umefunguliwa na wakili wa zamani wa Marekani, Michael Garcia ambaye aliteuliwa mwezi uliopita kuwa mkuu wa kitengo cha uchunguzi katika Kamati ya Maadili ya FIFA akishughulikia masuala ya rushwa. Bin Hammam ambaye pia amewahi kuliongoza Shirikisho la Soka barani Asia-AFC, tayari amesimamishwa tena kwa siku 90 ili kupisha uchunguzi huo kufanyika. FIFA inakusanya ushahidi zaidi juu ya tuhuma za zinamkabili Bin Hammam za kujaribu kuwanunua viongozi wa soka wa Caribbean ili waweze kumpigia kura katika uchaguzi wa shirikisho hilo uliopita. CAS ilitengua adhabu aliyopewa ya kufungiwa maisha aliyopewa Bin Hammam baada ya kukata rufani wakidai kuwa FIFA haikuwa na ushahidi wa kutosheleza kumtia hatiani Bin Hammam ingawa uamuzi haukumaanisha kwamba hakuwa na hatia hivyo kuifungua tena kesi hiyo kwa ajili ya kutafuta vielelezo vipya.
No comments:
Post a Comment