SAWA ATANGAZA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA.
|
Homare Sawa. |
NAHODHA wa timu ya taifa ya wanawake ya Japan, Homare Sawa anajipanga kustaafu kucheza soka ya kimataifa baada ya timu hiyo kuchukua medali ya fedha katika michuano ya olimpiki kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Marekani kwenye mchezo wa fainali uliofanyika juzi. Sawa mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikiongoza kikosi cha Japan kushinda taji la Kombe la Dunia mwaka jana nchini Ujerumani ataendelea kucheza soka katika ngazi ya klabu. Sawa ambaye ameichezea Japan michezo 186 na kufanikiwa kufunga mabao 81 amesema kuwa tayari amefanikiwa kupata kile alichoweza ingawa anakiri kuwa alikuwa akitaka na medali ya dhahabu kabla ya kustaafu lakini hilo halimuumizi kichwa kwani wataofuata wanaweza kufanikisha hilo. Mabao aliyofunga Sawa katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana yalikuwa chachu ya mafanikio kwa timu hiyo ambayo iliisambaratisha Marekani kwa changamoto ya mikwaju ya penati kwenye fainali iliyofanyika jijini Frankfurt.
No comments:
Post a Comment