MWENDESHA baiskeli nyota wa Uingereza, Sir Chris Hoy amenyakuwa medali ya sita ya dhahabu katika mbio hizo za olimpiki na mwingereza aliyefanikiwa zaidi katika michuano hiyo kweny kipindi chote. Dhahabu sita alizoshinda Hoy zinamfanya aongoze akimpita Sir Steve Redgrave ambaye alikuwa mpiga makasia nyota aliyenyakuwa medali tano huku akifikia rekodi ya Bradley Wiggins ya kuwa na medali saba ukijumuisha na medali ya fedha aliyoipata katika michuano iliyofanyika Sydney mwaka 2000. Hoy mwenye umri wa miaka 36 raia wa Scotland hataweza kupwepo katika michuano ya olimpiki mwaka 2016 kutokana na umri kuwa mkubwa lakini tayari ameshatengeneza jina na kuwa mwendesha baiskeli nyota kuwahi kutokea kutokana na umahiri aliouonyesha katika michuano ya mwaka huu. Katika mbio hizo Maximilian Levy wa Ujerumani alishika nafasi ya pili na kunyakuwa medali ya fedha huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Teud Mulder wa Uholanzi na Simon van Velthooven wa New ambao wote walivuka mstari pamoja hivyo kupew medali ya shaba.
Wednesday, August 8, 2012
HOY ANYAKUWA MEDAI YA SITA KATIKA BAISKELI NA KUWEKA HISTORIA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment