Wednesday, August 8, 2012

BRAZIL ONE STEP CLOSER TO THE GOLD.


 

NDOTO za timu y taifa ya Brazil kunyakuwa medali ya kwanza ya dhahabu ya michuano ya Olimpiki ina karibia kutimia baada ya jana kufanikiwa kuifunga Korea Kusini mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa katika Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester. Ushindi huo umeipeleka timu hiyo kukutana na Mexico katika mchezo wa fainali ambao utachezwa Jumamosi katika Uwanja wa Wembley baada ya timu hiyo ambayo nayo inatoka kusini mwa bara la Amerika kuisambaratisha Japan kwa mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali. Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wapatao 69,389 Brazil walipata bao la kuongoza katika dakika ya 38 kupitia kwa Romulo huku mengine mawili yakifungwa na Leandro Damiao katika kipindi cha pili na kufanya aongoze katika orodha ya wafungaji akiwa na mabao sita kwenye michuano hiyo. Brazil inapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa medali ya dhahabu katika michuano hiyo ambayo wamekuwa wakishiriki bila mafanikio kwa miaka zaidi ya 60 na kufanikiwa kunyakuwa medali za fedha katika michuano ya mwaka 1984 na 1988.

No comments:

Post a Comment