POWELL NJE OLIMPIKI.
|
Asafa Powell. |
MWANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Asafa Powell hatakuwepo na wenzake wakati wakitetea taji lao la mbio za kupokezana vijiti za mita 400 katika mochuano ya olimpiki jijini London kutokana na maumivu yanayomkabili. Powell aliumia wakati wa fainali za mbio za mita 100 na kumfanya kumaliza wa mwisho kwenye mbio hizo ambazo wenzake Usain Bolt na Yohan Blake walinyakuwa medali za dhahabu na fedha. Meneja wa Powell, Paul Doyle amesema kuwa nyota huyo itamchukua zaidi ya wiki tatu kupona maumivu ya msuli yanayomkabili. Katika mbio za kupokezana vijiti ambazo zinatarajiwa kufanyika Jumamosi sasa zinatarajiwa kuwa na nyota kama Bolt, Blake, Nesta Carter na Michael Frater ambao walishinda taji la dunia mwaka uliopita na kuweka rekodi ya dunia yam bio hizo. Maumivu hayo yanayomkabili Powell yatamfanya kutoshiriki michuano mingine kwa mwaka huu lakini anatarajia kurejea tena msimu wa 2013.
No comments:
Post a Comment