TANZANIA imeporomoka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 127 waliyokuwa mwezi uliopita mpaka nafasi 128 katika orodha za kila mwezi ubora zinazotolewa na Shrikisho la Soka Duniani-FIFA. Katika orodha hizo mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania imeendelea kujikita katika nafasi ya kwanza katika msimamo huo wakifuatiwa na Ujerumani huku Uingereza wakipanda kwa nafasi moja pamoja na kutolewa mapema katika michuano ya Ulaya. Nafasi ya nne katika orodha hizo inashikiliwa na Uruguay ambao wameporomoka kwa nafasi moja wakifuatiwa na Ureno katika nafasi ya tano, Italia nafasi ya sita, Argentina nafasi ya saba, uholanzi nafasi ya nane, Croatia nafasi ya tisa na Denmark nafasi ya 10. Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil wana kazi ya ziada ya kufanya kuhakikisha wanarejesha makali yao kwani wamezidi kuporomoka katika viwango hivyo kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya 13. Kwa upande wa Afrika Ivory Coast imeendelea kuongoza kwa kukamata nafasi ya 16 katika orodha hizo wakifuatiwa na Ghana ambao wako katika nafasi ya 32 huku wa tatu wakiwa Algeria ambao wako katika nafasi ya 34. Nafasi ya nne kwa Afrika inashikwa na Libya nafasi ya 38 wakifuatiwa na Mali nafasi ya 39 na Misri nafasi ya 40 wakati mabingwa wa Afrika Zambia wakizidi kuporomoka kwa nafasi tatu mpaka 44.
Wednesday, August 8, 2012
TANZANIA YAPOROMOKA NAFASI MOJA VIWANGO FIFA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment