Tuesday, August 7, 2012

KISIWA CHA GRENADA CHATANGAZA SIKU YA MAPUMZIKO BAADA YA MWANARIDHA WAKE KUSHINDA MEDALI YA DHAHABU KATIKA OLIMPIKI.

Kirani James wa pili kutoka kulia akimaliza mbio za mita 400.
JANA ilikuwa ni siku ya furaha kwa kisiwa cha Grenada kilichopo Caribbean baada ya mwanariadha Kirani James kunyakuwa medali ya dhahabu katika mbio za mita 400 kwenye michuano ya olimpiki jijini London. Wananchi wa Grenada walikuwa akicheza, kushangilia na kupeperusha bendera katika mitaa ya nchi hiyo wakati James mwenye umri wa miaka 19 aliposhinda medali ya kwanza ya dhahabu kwa nchi hiyo akitumia muda wa sekunde 43.94. Waziri Mkuu wa nchi hiyo Tillman Thomas alitangaza siku ya Jumanne kuwa ya mapumziko kiserikali huku akimwelezea mwanariadha huyo kama mfano wa kuigwa na vijana wengine wan chi hiyo. Thomas alimsihi James kuendelea kufanya vizuri zaidi katika michuano mingine ili kuliwakiisha vyema taifa hilo na kuendelea kudumisha nidhamu ili aweze kufanikiwa. Watu wa Grenada wanategemea ushindi wa James utakuza jina la taifa hilo ambalo lina idadi ya watu zaidi ya 100,000 na uchumi mkubwa ukitegemea sekta ya utalii.

No comments:

Post a Comment