Tuesday, August 7, 2012

MSERBIA BUNJAK KOCHA MPYA AZAM FC.

Boris Bunjak.
TIMU ya Azam imempa mkataba wa miaka miwili kocha mpya Boris Bunjak kutoka Serbia ambaye atarithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Stewart Hall kutoka Uingereza. Stewart alitimuliwa kibarua cha kuinoa klabu hiyo Jumatano iliyopita kufuatia kikao cha bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo baada ya kukiuka masharti aliyopewa na bodi hiyo ya kutompanga mchezaji Mrisho Ngassa katika mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi Makamu Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed amesema kuwa baada ya bodi pamoja na menejimenti wa klabu hiyo kupitia wasifu wa makocha ambao walikuwa wametuma maombi ya kuinoa klabu hiyo waliridhishwa na wasifu wa Bunjak. Mohamed aliendelea kusema kuwa Bunjak mwenye umri wa miaka 54 ambaye ana cheti cha ukocha kinachotambulika na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA amewahi kufundisha vilabu 15 tofauti barani Asia na Ulaya na hii ni mara ya kwanza kufundisha Afrika. Akihojiwa mara baada ya utambulisho huo Bunjak amesema kuwa amefurahi kuteuliwa kuifundisha klabu hiyo kwasababu ni klabu yenye uchu wa mafanikio na kutwaa mataji mengi zaidi. Mohamed amesema kuwa kocha Vivek Nagul kutoka India ambaye alikuwa anakaimu nafasi ya Stewart ataendelea kuwa kocha wa vijana wakati msaidizi wa Bunjak atabakia kuwa Kalimangonga Ongala.

No comments:

Post a Comment