Thursday, August 16, 2012

MESSI, RONALDO WASAIDIA TIMU ZAO ZA TAIFA KUSHINDA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Argentina Lionel Messi alifanikiwa kuingoza vyema timu yake kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jana. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali juu Messi alifunga bao moja huku akikosa bao lingine baada ya kupaisha mkwaju wa penati aliopiga. Michezo mingine ya kirafiki iliyochezwa jana usiku Uholanzi walishangazwa na Ubelgiji baada ya kutandikwa mabao 4-2 huku Ufaransa ambayo inanolewa na kocha mpya Didier Deschamp ikishindwa kuitambia Uruguay nyumbani kwa kutoka nayo sare ya mabao bila kufungana.
rusi ambayo inanolewa na kocha wa zamani wa Uingereza Fabio Capello ilishindwa kutamba mbele ya Ivory Coast kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 huku mabingwa wa Dunia na Ulaya, Hispania wenyewe walipata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 kwa timu dhaifu ya Puerto Rico mabao ambao yalifungwa na Santi Carzola na Cesc Fabregas. Baadhi ya michezo mingine mikubwa iliyochezwa jana Uingereza ilifanikiwa kuifunga Italia kwa mabao 2-1, Portugal waliifunga Panama mabao 2-0 wakati mabingwa wa dunia mara tano Brazil walisahau mchezo wa fainali ya olimpiki waliopoteza na kufanikiwa kuifunga Sweden mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment