Sunday, August 19, 2012

PARDEW AOMBA RADHI KWA KUMSUKUMA MWAMUZI.

MENEJA wa klabu ya Newcastle United Alan Pardew ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumsukuma mwamuzi msaidizi wakati wa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Uingereza ambao timu yake iliibuka kidedea dhidi ya Tottenham Hotspurs. Penati ya dakika za mwisho iliyopigwa na Hatem Ben Arfa iliwahakikishia alama zote tatu baada Jarmain Defoe kumkwatua Demba Ba katika eneo la hatari. Lakini Pardew alitolewa katika benchi la ufundi na kupelekwa jukwaani baada ua kumsukuma mshika kibendera Stuart Burt wakati akilalamika kuhusu mpira uliotoka nje wakati timu yake ikishambuliwa na Spurs katika mchezo huo. Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha huyo alimfuata mwamuzi na kumwomba radhi kabla ya kuomba radhi pia kwa mashabiki kwa kitendo chake kisicho cha uanamichezo alichokionyesha. Kama tukio hilo likitajwa katika taarifa ya itakayowasilishwa na mwamuzi Martin Atkinson, Pardew anaweza kutozwa faini au kufungiwa.

No comments:

Post a Comment