Sunday, August 19, 2012
MODRIC HATIHATI KUONDOKA SPURS.
KIUNGO wa klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza Luka Modric ana wasiwasi kuwa uhamisho wake wa paundi milioni 35 kwenda klabu ya Real Madrid ya Hipsnia unaweza kukwama. Spurs ambao wanaonekana kutopendezwa na suala la kumuuza mchezaji huyo wamemwambia kuwa hawataweza kumuuza kwa bei rahisi kama hiyo ambayo Madrid wamepanga kutoa. Katika mazungumzo ambayo yalifanywa na meneja wa Madrid Jose Mourinho na bosi wa Spurs Daniel Levy walionekana kutofikia muafaka baada ya Levy kudai nyongeza ya paundi milioni mbili katika dakika za mwisho. Mourinho ambaye amewahi kuifundisha Chelsea anapanga kujitoa katika mbio za kumfukuzia kiungo huyo na kwenda kutafuta mchezaji mwingine wa aina yake na kumuacha Modric akiwa katika hali ya sintofahamu. Modric ambaye ni raia wa Croatia amekuwa akitamani kuondoka Spurs kwa kipindi kirefu na alikuwa kiamini kuwa msimu huu ndio ulikuwa muafaka kwake kuondoka lakini inaonekana kama anaweza kuendelea kuwepo kwa msimu mwingine tena. Kocha wa Spurs Andre Villas-Boas amesema suala la Modric amemuachia mwenyekiti wa klabu hiyo alimalize na kama akishindwa kumuuza basi atamrejesha katika kikosi chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment