AL AHLY YAANZA VISINGIZIO.
BENCHI la Ufundi la timu ya Al Ahly ya Misri imeonyesha kuogopeshwa baada ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kumteua mwamuzi Salim El Gadedi kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi Zamalek. Al Ahly wanaamini kuwa mwamuzi anaweza kuwapa wakati mgumu katika mchezo huo haswa baada ya kushuhudia akigawa kadi za njano kama njugu katika michezo miwili iliyopita ambayo alikuwa akipuliza kipenga. Katika mchezo huo Al Ahly ambao watakutana na mahasimu wao Zamalek wanataka kushinda mchezo huo ili waweze kuongoza kundi lao na kuikwepa timua ya Esperance ya Tunisia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Mtanange baina ya timu hizo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Borg Al Arab uliopo jijini Alexadria Jumapili Septemba 16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment