Friday, September 14, 2012
UCHUNGUZI WA VIFO VYA HILLBOROUGH WAANZA UPYA.
POLISI wa mji wa Kusini mwa Yorkshire wamefungua upya tena uchunguzi katika kikosi chake kufuatia maafa yaliyotokea mwaka 1989 huko Hillsborough, Uingereza. Hatua hiyo imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa kuwa maofisa wa polisi walibadilisha maelezo na kujaribu kuwatupia lawama mashabiki wa klabu ya Liverpool kufuatia tukio hilo la mwaka 1989 ambalo liliua watu 96. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea kutokana na mashabiki kujaa uwanjani kupita uwezo na kuanza kukanyagana wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA uliochezwa April 15 mwaka 1989. Jumatano kamati huru ambayo iliundwa kuchunguza tukio la Hillsborough ilitoa taarifa hiyo baada ya kutumia zaidi ya miaka miwili kupitia nyaraka zaidi 400,000 kuhusiana na tukio hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment