MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Uingereza tena baada ya kupata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Southampton Jumamosi. Arsenal walionyesha soka safi na la kuvutia wakati wa kipindi cha kwanza mashabulizi ambayo yalikuwa yakiongozwa na wachezaji wapya wa klabu hiyo Santi Cazorla na Lukas Podolsky. Akihojiwa Wenger amesema kuwa timu yake hiyo ina nafasi ya kunyakuwa taji hilo lakini inabidi kwanza wachezaji wake waonyeshe kama kweli wanalihitaji kwa kucheza katika kiwango cha juu katika michezo inayofuata. Arsenal ambao mara ya mwisho kunyakuwa taji ilikuwa mwaka 2004, wako alama mbili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Chelsea huku wakiwa wameruhusu wavu wao kutikiswa mara moja katika michezo minne waliyocheza mpaka sasa.
No comments:
Post a Comment