MCHEZAJI ambaye maofisa wa soka nchini Australia wanaamini kuwa atasaidia kuleta muamko mpya katika mchezo huo ametua nchini humo leo kuanza rasmi mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Sydney FC. Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia na klabu ya Juventus, Alessandro Del Piero alitua nchini humo akiwa amevaa kitambaa cha timu Sydney na kupokewa na mamia ya mashabiki ambao walikuwa wakimsubiri uwanjani hapo kwa muda wa zaidi ya masaa matano. Del piero mwenye umri wa miaka 37 alionekana uwanjani hapo akiwa na familia yake ambapo inaripotiwa kuwa atakuwa akilipwa kiasi cha dola milioni mbili kwa mwaka katika mismu miwili atakayokuweo nchini humo. Mashabiki wengi waliojitokeza uwanjani hapo walikuwa wamevaa jezi namba 10 ambayo alikuwa akivaa wakati yuko Juventus wakati wengine wakiwa na mabango yakimuonyesha akiwa amevaa jezi ya klabu yake hiyo ya Italia ambayo ameichezea kwa kipindi cha miaka 19.
No comments:
Post a Comment