BEKI wa klabu ya Queens Park Rangers, Les Ferdinand amepuuza kupeana mkono na nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry kabla ya mchezo baina ya timu hizo uliopigwa katika Uwanja wa Loftus Road ambapo timu hizo zilitoka suluhu ya bila ya kufungana. Beki huyo ambaye ni ndugu na Rio Ferdinand wa Manchester United pia alikataa kumpa mkono beki wa kushoto wa Chelsea Ashley Cole wakati wachezaji hao wakisalimiana kabla ya mchezo huo. Chanzo kimoja ambacho kiko karibu na mchezaji huyo kimesema kuwa mchezaji huyo alishaamua kitambo kwamba hatakuja kushikana mikono na wachezaji hao kutokana na tabia zao walizozionyesha kwake. Hiyo sio mara ya kwanza kwa Ferdinand na Terry kukutana uwanjani toka hukumu ya kesi ambayo ilikuwa ikimkabili Terry kuhusiana na ubaguzi ilipotolewa Julai mwaka huu ambapo ilimkuta hana hatia lakini bado kuna uchunguzi wa Chama cha Soka cha nchi hiyo unaendelea kuhusiana na makosa hayo.
No comments:
Post a Comment