Saturday, September 1, 2012

JAPAN KUPEPETANA NA BRAZIL.

MABINGWA wa soka barani Asia Japan inatarajiwa kuchez mchezo wa kimataifa wa kirafiki na Brazil mchezo ambao utafanyika barani Ulaya, ikiwa ni mipango ya kocha wa Japan Alberto Zaccheroni ambaye anataka kujaribu kikosi chake na moja ya timu bora duniani. Chama cha Soka cha Japan-JFA kimesema kuwa kikosi cha nchi hiyo kitamenyana Brazil ambao ni mabingwa mara tano ya Kombe la Dunia jijini Wrocklaw, Poland Octoba 16 mwaka huu ikiwa ni siku nne baada ya kucheza na Ufaransa jijini Paris. Zaccheroni ambaye anapambana kuivusha Japan iweze kushiriki fainali zake nne za Kombe la Dunia mwaka 2014 amesema kuwa amefurahishwa na kupata michezo hiyo miwili migumu ya kirafiki. Michezo hiyo miwili itakuja kabla ya timu hiyo kumaliza mzunguko wake wa mwisho wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa upande wa bara ya Asia huku wao wakiwa wanaongoza kundi lao kwa alama saba baada ya kucheza michezo mitatu.

No comments:

Post a Comment