Saturday, September 1, 2012

MADRID YAMCHUKUA ESSIEN KWA MKOPO.

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imetangaza kufikia makubaliano ya kumnyakuwa kiungo wa Chelsea Michael Essien kwa mkopo katika kipindi chote cha msimu huu. Essien mwenye miaka ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2005 akitokea klabu ya Olympique Lyon ya Ufaransa anatua Madrid na kukutana na Jose mourinho ambaye amewahi pia kuinoa klabu hiyo ya Uingereza. Mchezaji huyop anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji akiwa na Chelsea amefanikiwa kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu nchini humo, mataji manne ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Essien hakuwemo katika kikosi cha Chelsea ambacho kilichabangwa mabao 4-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa Super Cup uliochezwa jijini Monaco, Ufaransa jana usiku.

No comments:

Post a Comment