Thursday, September 13, 2012

MOROCCO NA KIPIGO CHA MABAO 2-0 KUTOKA KWA MSUMBIJI.

IKIWA siku tatu zimepita toka timu ya taifa ya Morocco ikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Msumbiji mwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 kumekuwa na kelele nyingi nchini na kutaka kuondolewa kwa kocha wa timu hiyo Eric Gerets. Mashabiki, maofisa na wachezaji wa zamani wan chi hiyo akiwemo Moustapha Hadji wamekuwa wakizungumza kuiomba wizara ya michezo na shirikisho la soka nchini humo kuvunja mkataba na kocha huyo raia wa Ubelgiji wakimlaumu kwa kupanga wachezaji ambao hawakustahili katika mchezo huo. Waziri wa Michezo wa nchi hiyo Mohamed Ouzzine alimkingia kifua kocha huyo ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2014 kufuatia kipigo hicho walichopata na kudai kuwa pamoja na kipigo hicho lakini timu hiyo itafanikiwa kusonga mbele. Ouzzine aliendelea kusema kuwa lawama za kipigo hicho wanazibeba wao viongozi na kuwaomba mashabiki wa soka nchini humo kutulia na kumpa nafasi Gerets kwani ana kazi ya kumalizia.

No comments:

Post a Comment