Thursday, September 13, 2012

URUSI KUENGUA MIJI MIWILI.

URUSI inatarajia kupunguza miji miwili kati ya 13 ambayo imeomba ridhaa kuandaa baadhi ya mechi za michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Akitaja miji ambayo inaweza kuwa katika hatari hiyo ya kuondolewa mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano hiyo nchini humo Vitaly Mutko amesema kuwa miji hiyo ni pamoja na Saransk, Volvograd, Yaroslavl, Kaliningrad na Rostov. Akizungumza na waandisi wa habari, Mutko ambaye pia ni waziri wa michezo nchini humo amesema kuwa kwasasa wana viwanja 15 ambavyo vipo katika miji 13 lakini wenyewe wamepanga kutumia viwanja 12 katika miji 11 hivyo itawabidi kupunguza miji miwili. Kamati hiyo inatarajia kutangaza miji wenyeji Septemba 29 mwaka huu wakati ambao watakuwa wamemaliza kuifanyia usaili miji hiyo.

No comments:

Post a Comment