Monday, September 17, 2012

WILSHERE KUREJEA UWANJANI KARIBUNI.

KIUNGO wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere anatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Arsenal Wenger wakati atakapoanza rasmi mazoezi na klabu hiyo wiki hii. Wilshere mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yamesababisha kuwa nje ya uwanja toka Agosti mwaka 2011 lakini kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kusahau yote hayo na kurejea uwanjani tena. Nyota alikuwa tayari ameanza mazoezi mepesi na kuonyesha maendeleo mazuri hivyo anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mazoezi mwishoni mwa wiki hii. Klabu imepanga kujaribu kumchezesha kiungo huyo katika baadhi ya michezo ya kirafiki mazoezini au katika kikosi cha timu hiyo cha vijana chini ya miaka 21 ambacho kitapambana na West Bromwich Octoba mosi ili kujaribu kumrejesha katika kiwango chake cha awali.

No comments:

Post a Comment