Wednesday, October 3, 2012
AFRICAIN YATAKA HUDUMA YA SHEHATA.
KLABU ya Africain ya nchini Tunisia imeonyesha nia kutaka kumuajiri kocha wa zamani wa Zamalek ya Misri, Hassan Shehata ili kukinoa kikosi cha timu hiyo. Mapema klabu hiyo ilikatisha mkataba na aliyekuwa kocha wake Bernard Casoni ambaye ni raia wa Ufaransa kwa kile walichodai matokeo mabaya ambayo imekuwa ikipata timu hiyo katika michezo yake ya karibuni. Taarifa kutoka nchini Tunisia zinasema kuwa mbali na Shehata lakini pia kocha wa zamani wa klabu ya Al Ahly Manuel Jose aliwekwa katika orodha lakini Shehata ndiye aliyeibuka kidedea. Wakati Shehata akikataa kutoa kauli kuhusiana na hilo, kuna taarifa kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kuchukua kibarua hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment