Wednesday, October 3, 2012

FIFA YAMSIMAMISHA OFISA WA BIN HAMMAM.

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limemsimamisha ofisa mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi na Mohamed Bin Hammam baada ya kugoma kutoa ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya bosi wake huyo wa zamani. Najeeb Chirakal ambaye alikuwa anafanya kazi katika Chama cha Soka nchini Qatar amefungiwa na kamati hiyo kwa miezi miwili au mpaka hapo atakapoamua kutoa ushirikiano katika uchunguzi huo. Katika taarifa yake waliyotuma katika mtandao kamati hiyo imesema kuwa Chirakal atafungiwa kwa miezi miwili au mpaka atapoamua kutoa ushirikiano kwa baadhi ya taarifa zinazohitajika katika uchunguzi huo. Bin Hammam anachunguzwa kutokana na tuhuma za utoaji rushwa wakati wa kampeni za kugombea kiti cha urais wa FIFA mwaka jana nafasi ambayo alishinda Sepp Blatter. Mbali na uchunguzi huo pia Bin Hammam mwenye umri wa miaka 63 raia wa Qatar pia anachunguzwa na Shirikisho la Soka barani Asia juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha wakati akiwa rais wa shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment