Wednesday, October 3, 2012

PUYOL KUIKOSA EL CLASICO.

BEKI wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Carles Puyol amekimbizwa hospitali baada ya kuteguka kiwiko cha mkono wake wa kulia wakati timu yake iliopibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Benfica katika mchezo wa kundi G wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jana. Kuumia kwa mchezo huyo ambaye ndio alikuwa akicheza kwa mara ya kwanza toka apone maumivu ya mguu yaliyokuwa yakimsumbua kutapelekea kukosa mchezo dhidi ya mahasimu wao Real Madrid utakaochezwa Jumapili katika Uwanja wa Nou Camp. Puyol mwenye umri wa miaka 34 alidondoka vibaya na kuumiza kiwiko chake wakati akiwa katika harakati ya kuwania mpira wa kona ambapo alitolewa nje katika dakika ya 78 na nafasi yake kuchukuliwa na Alex Song. Meneja wa Barcelona Tito Vilanova amesema kuwa wanasubiri vipimo vya madaktari ili kujua mchezaji huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini inavyoonekana atakosa mchezo wa Jumapili dhidi ya Madrid. Barcelona imekuwa ikiyumba katika safu yake ya ulinzi katika siku za karibuni baada ya mabeki wake tegemeo kuumia mara kwa mara ambapo Gerard Pique bado yuko nje ya uwanja kutokana akijiuguza kutokana na majeraha waliyopata.

No comments:

Post a Comment