GHANA imekuwa nchi ya kwanza kukata tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika itakayochezwa mapema mwakani baada ya kufanikiwa kuifunga Malawi kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa jinni Lilogwe Jumamosi mchana. Bao la Ghana ambao pia wanajulikana kama Black Stars lilifungwa katika dakika za mwanzoni na Agriyie Acquah na kuifanya timu hiyo kuibika na ushindi wa mabao 3-0 katika michezo miwili ambayo walikutana. Mbali na mchezo huo mabingwa wa Afrika Zambia nao walifanikiwa kukata tiketi baada ya kuifunga Uganda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-9 jijini Kampala baada ya wenyeji kufanikiwa kushinda bao 1-0 katika dakika za kawaida. Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo ambao ulichezwa jijini Lusaka, wenyeji walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Michezo mingine ya kufuzu mataifa ya Afrika iliyochezwa jana Botswana ilishindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Mali, Nigeria iliigaragaza Liberia kwa mabao 6-1. Tunisia ilitoka sare ya bila ya kufungana na Sierra Leone, Morocco iliifunga Msumbiji kwa mabao 4-0 wakati Senegal ilishindwa kutamba mbele ya Ivory Coast baada ya kufungwa mabao 2-0 katika mchezo ulioisha kwa vurugu.
No comments:
Post a Comment