CHAMA cha Soka nchini Uingereza, kimesema kuwa mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya nchi hiyo Theo Walcott ameondolewa katika kikosi cha timu hiyo ambacho kitapambana Poland katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia jijini Warsaw Jumanne ijayo. Walcott alipamiwa na golikipa wa San Marino Aldo Simoncini dakika tano kabla ya mpira kumalizika ambapo Uingereza ilishinda kwa mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Wembley na kulazimika kupumzishwa hospitalini kwa ajili ya uangalizi maalumu. Kocha wa Uingereza Roy Hodgson alionyesha kuchukukizwa na rafu aliyocheza Simoncini na kushinikiza kuwa golikipa kipa alistahili kupewa kadi nyekundu katika mchezo huo. Kuumia kwa Walcott itakuwa ni pigo kubwa katika kikosi hicho cha Uingereza kutokana na mchezo mgumu dhidi ya Poland uliokuwepo mbele yao.
No comments:
Post a Comment