Kiungo wa AC Milan MASSIMO AMBROSINI na beki wa Inter Milan YUTO NAGATOMO ni miongoni mwa wachezaji sita waliofungiwa mechi na maofisa wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A. AMBROSINI hakujumuishwa katika kikosi cha AC Milan ambacho kilifungwa na Inter kwa bao 1-0 Jumapili lakini alifungiwa kutokana na tukio lake la kunyanyuka kutoka benchi la wachezaji wa akiba na kusogea karibu na uwanja kuonyesha hasira zake dhidi ya maamuzi ambayo yalikuwa yamefanywa na mwamuzi wa mchezo huo katika dakika ya 47. NAGATOMO naye alifungiwa mchezo mmoja kufuatia kuonywa kutokana na mchezo mbaya katika kipindi cha kwanza na baadae alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kufuatia kuunawa mpira kwa makusudi dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza. Wachezaji wengine waliofungiwa mechi moja ni pamoja na YOHAN BENALOUANE na ALESSANDRO LUCARELLI ambao wote wanacheza katika timu ya Parma mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil ZE EDUARDO ambaye anacheza Siena na Beki wa Torino MATTEO DARMIAN.
No comments:
Post a Comment