Friday, October 12, 2012

APPIAH ATAMBA KUSHINDA KAMPALA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana, Kwesi Appiah amesifu kikosi chake kwamba kimejipanga vizuri kwa mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 dhidi ya Malawi mchezo ambao utachezwa baadae leo. Appiah alitamba kuwa amewaita wachezaji wote nyota walioko nje kwa ajili ya mchezo huo wakati alifafanua sababu ya kumuacha kiungo wa Udinese Emmanuel Agymang-Badu kwamba ana matatizo ya kifundo cha mguu. Mbali na mchezo huo pia kuna michezo mingine ambapo mabingwa mara nne wa Afrika Cameroon wataikaribisha Cape Verde jijini Younde katika mchezo ambao utakuwa ni wa kufa na kupona kwa mabingwa hao baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Zambia nao watakuwa na kibarua kigumu jijini Kampala pale watapokwaana na Uganda baada yakupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Lusaka.

No comments:

Post a Comment