
Friday, October 12, 2012
GAMAL ALLAM MWENYEKITI MPYA FA YA MISRI.
GAMAL Allam amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama cha Soka nchini Misri-EFA kwa kipindi cha miaka minne ijayo. Wajumbe wa EFA walimchagua Allam kwa kura 110 kuongoza chama hicho na kuwabwaga wapinzani wake ambao ni Ihab Saleh aliyepata kura 41 na Usam Khalil aliyepata kura 39 katika uchaguzi uliofanyika chini ulinzi mkali wa polisi. EFA itaongozwa na Allam pamoja na wajumbe 10 wa bodi ambao ni Hassan Farid, Ihab Laheta, Ahmed Mogahed, Mahmoud El Shami, Essam Abd El Fatah, Hamada El Masry, Magdy El Metnawy, Saif Zaher, Khaled Latif na Sahar El Hawary. Allam anaziba nafasi ya Samir Zaher ambaye alijiuzulu wadhfa huo kufuatia vurugu zizlizotokea Port Said Februari mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment