Friday, October 12, 2012

ROBSON ASHINDWA KUTAMBA JAPAN.

MCHEZAJI tenisi nyota wa Uingereza, mwanadada Laura Robson ameshindwa kutinga nusu fainali ya michuano ya wazi ya Japan baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Chang Kai-chen wa Taipei katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jijini Osaka. Robson ambaye anashika namba nane katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanawake alishindwa kutamba katika robo fainali hiyo baada ya kukubali kipigo cha seti 2-1 zenye alama za 6-3 3-6 7-6. Kwa upande wa mwanadada mwingine kutoka Uingereza Heather Watson mambo yalimyookea baada ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa kumchapa Pauline Parmentier wa Ufaransa kwa seti 2-0 zenye alama za 7-5 6-3. Ushindi huo unamhakikishia Watson kumaliza msimu akiwa katika orodha ya wachezaji 60 bora wa michuano hiyo na sasa atakwaana na Misaki Doe wa Japan ambaye nae alimsambaratisha Chanelle Scheepers kwa seti 2-1 zenye alama za 2-6 6-1 6-3.

No comments:

Post a Comment