Friday, October 12, 2012
DAVIDS KUWA KOCHA MCHEZAJI KATIKA TIMU YA BARNET.
MCHEZAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Edga Davids ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Ligi Daraja la pili ya Barnet akiwa na Mark Robson ambapo mbali ya kuwa kocha nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 pia atakuwa mchezaji. Timu hiyo kwasasa iko katika nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imejikusanyia alama tatu pekee katika michezo 11 waliyocheza hivyo ujio wa Davids unategemewa kuinua timu hiyo ili isihishuke daraja. Alhamisi usiku nyota huyo alituma ujumbe katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kuonyesha furaha yake ya kujiunga na klabu hiyo kama kocha mchezaji na kuomba ushirikiano ili waweze kupata mafanikio akiwa hapo. Davids pia alituma picha katika twitter ambayo alipiga pamoja na Mwenyekiti wa klabu hiyo Anthony Kleanthous, Robson pamoja na meneja wa zamani ambaye kwasasa ni Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Paul Fairclough. Davids ambaye anacheza nafasi ya kiungo amewahi kucheza katika vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Barcelona, Juventus, Ajax na AC Milan.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment