Friday, October 12, 2012

NGULI WA UJERUMANI AFARIKI DUNIA.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani, Helmut Haller ambaye alifunga bao katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 na mjerumani wa kwanza kucheza soka nchini Italia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73. Haller alifariki dunia nyumbani kwake katika mji wa Augsburg kwa ugonjwa wa kichaa au dementia ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda mrefu. Haller aliifungia Ujerumani bao la kuongoza katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 fainali ambayo hata hivyo Uingereza ndio waliibuka washindi na kunyakuwa kombe hilo. Nguli huyo ameichezea Ujerumani michezo 33 na kufunga mabao 13 pia amcheza katika fainali mbili zaidi za michuano ya Kombe la Dunia la mwaka 1962 na 1970. Haller ni mmoja ya wajerumani wa kwanza kwenda kucheza soka nje ya nchi hiyo ambapo alicheza soka nchini Italia kwa miaka 11 akishinda mataji matatu ya Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Serie A akiwa na klabu za Bologna na Juventus.

No comments:

Post a Comment