Wednesday, October 31, 2012

ARSENAL 7 READING 5.

KLABU ya Arsenal jana imefanikiwa kupigana kiume baada ya kuwa nyuma kwa mabao 4-0 mpaka muda wa mapumziko na kufanikiwa kushinda kwa mabao 7-5 katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Reading katika Uwanja wa Madejski. Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alikaririwa wiki iliopita akisema kuwa michuano hiyo anaipa umuhimu wa mwisho katika malengo yake msimu huu ambapo kauli yake ingetimia kama ukuta wa Reading ungekuwa imara baada ya timu hiyo kuongoza kwa mabao 4-0 katika dakika 37 za mchezo huo. Mara baada ya ushindi huo Reading ambao wanashika wanashika nafasi ya tatu kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza walishindwa kuhimili vishindo vya Arsenal baada ya nyota wake Theo Walcott kuipatia bao la kuongoza kabla ya mapumziko na baadae kufunga mengine mawili. Wenger aliwapongeza vijana wake kwa kutokata tamaa pamoja na kukubali wavu wao kutikiswa mara nne na kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mchezo huo muhimu.

No comments:

Post a Comment