Wednesday, October 31, 2012

FA YASUBIRI TAARIFA KUTOKA SERBIA JUU YA KUFUNGIWA WACHEZAJI WAKE KUTOKANA NA VURUGU.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kimethibitisha kuwa hawajapewa taarifa juu ya uamuzi wa maofisa wa polisi nchini Serbia kuwahusisha wachezaji wawili wa timu ya taifa chini ya miaka 21 ya Uingereza kwa vurugu. Shirikisho la Soka nchini Serbia liliwafungia viungo Nokla Ninkovic na mshambuliaji Ognjen Mundrinski kucheza katika timu za taifa lakini mamlaka ya kisheria ilitangaza kuwashitaki watu 12 katika vurugu hizo yakiwemo majina mawili ya Uingereza. Katika taarifa ya FA ilithibitisha kuwa hawajapata taarifa rasmi zozote kuhusu kufungiwa kwa wachezaji wake na shirikisho la soka ya Serbia na kwamba wanasubiri maelezo zaidi kuhusiana na sakata hilo. Taarifa hiyo ilimalizwa kwa kusema FA itawapa msaada wachezaji pamoja na viongozi waliokumbana na sakata hilo nchini Serbia wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment