Wednesday, October 31, 2012

DJOKOVIC AJIHAKIKISHIA KUMALIZA NAMBA MOJA.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Serbia, Novak Djokovic amejihakikishia nafasi ya kumpita mpinzani wake Roger Federer na kumaliza mwaka 2012 akiwa kinara katika orodha za ubora duniani kwa upande wa wanaume. Djokovic alipoteza nafasi yake hiyo kwa Federer mwenye umri wa miaka 31 baada ya kunyakuwa michuano ya Wimbledon lakini Federer ambaye anatoka Switzerland hataweza kutetea taji la Paris Masters. Kutokuwepo kwa Federer katika michuano hiyo mikubwa ya dunia ya mwisho kwa mwaka huu ambayo itafanyika Novemba 5 kunampa nafasi Djokovic kurejea katika kiti chake. Djokovic mwenye umri wa miaka 25 anakuwa nyota wa kwanza kumaliza mwaka katika nafasi ya kwanza mfululizo toka Federer alipofanya hivyo kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007.

No comments:

Post a Comment