Thursday, October 18, 2012

AYEW APEWA SIKU SABA ZA KUOMBA RADHI.

MCHEZAJI nyota wa timu ya taifa ya Ghana, Andre Ayew amepewa siku saba za kuomba msamaha na Shirikisho la Soka la nchi hiyo-GFA baada ya kutupa kitambaa cha mkononi kuonyesha hasira zake kwa kutolewa katika mchezo dhidi ya Malawi mwishoni mwa wiki. Akihojiwa na redio moja nchini Ghana rais wa GFA Kwesi Nyantakyi amesema katika kikao walichokaa walifikia maamuzi ya kumpa wiki moja Ayew aombe radhi kwa uma kutokana na kitendo chake hicho na kama hata fanya hivyo watamchukulia hatua zinazohusika. Waandishi waliokuwa wakiripoti mchezo huo wamebainisha kwamba mara baada ya kutolewa mchezaji huyo alionyesha kukasirika kwani alishindwa hata kuwa mkono wachezaji wenzake waliokuwepo katika benchi la wachezaji wa akiba ingawa mwenye hajasema lolote kuhusiana na hilo. Kocha wa timu hiyo Kwesi Appiah pamoja na benchi lake la ufundi nao pia hawajazungumzia lolote kuhusiana na tukio la mchezaji huyo kwa kuwaachia GFA watoe uamuzi wanaouona ni sahihi.

No comments:

Post a Comment