Thursday, October 18, 2012

UEFA KUZICHUKULIA HATUA YA KINIDHAMU SERBIA NA UINGEREZA.

SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA limefungua mashtaka ya kinidhamu kwa nchi za Serbia na Uingereza na kuamuru uchunguzi wa polisi juu ya tuhuma za ubaguzi zilizotokea katika mchezo wa baina ya nchi hizo wa vijana chini ya miaka 21. Wenyeji wa mchezo Serbia wamefunguliwa mashtaka na UEFA juu ya matukio ya ubaguzi wa rangi yaliyoonyesha na mashabiki wake kwenda kwa wachezaji weusi wa Uingereza kabla ya mchezo huo uliochezwa Jumanne usiku. Lakini pia vyama vya soka vya nchi zote mbili navyo vimeshtakiwa kwa kushindwa kuzuia vurugu ambazo zilitokea uwanjani mara baada ya mchezo huo kumalizika ambapo Uingereza ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Mashtaka hayo yanatarajiwa kusikilizwa na bodi ya nidhamu ya UEFA Novemba 22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment